Fahamu zaid juu ya Afya- magonjwa, tiba na ushauri. Pia pata elimu sahihi ya ujasiriamali

Monday 18 April 2016

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO IMEPATIKANA!!!

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO IMEPATIKANA!!!

VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)
Habari za siku mpenzi msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia blog yangu iwapo una maoni au chochote unaweza kuwasiliana Nami, pamoja na hayo leo ninazungumzia ugonjwa hatari unaowanyima raha wengi wetu kutokana na Hali halisi hivyo kuwafanya watu  kuwa wazito kutafuta dawa,
VIDONDA VYA TUMBO NI NINI???
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri
_vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu,
_vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika  koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo
_ni Ajabu tu kwamba kimelea cha HELICOBACTER PYLORI kina uwezo wa kuishi ndani ya tumbo la Chakula licha ya  tindikali iliyomo katika tumbo ni kali sana, kiasi kimelea hiki kisingeweza kuishi tumboni ila kuna sababu za kisayansi zinazofanya kimelea hiki  kustahimili tindikali na kusababisha vidonda vya tumbo

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)
Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo navyo ni
 (a) GASTRIC ULCERS ~hivi ni vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni
b) DUODENAL ULCERS ~hivi ni vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo
 (c) OESOPHAGEALS ULCERS~hivi ni vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula
HATUA KUU  ZA VIDONDA VYA TUMBO
ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu
(@)HATUA YA KWANZA ~hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo,
(@)HATUA YA PILI~hapa vijidonda hujitokeza   sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hvyo huongezeka na kua vikubwa  katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu, hata hvyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kaz kwa mfumo wa mmeng'enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa dam hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu
(@)HATUA YA TATU ~hii ni hatua ambayo ni ya  hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.
(@)HATUA YA NNE ~katika hatua saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo
VISABABISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na huu ugonjwa.zifuatazo ni visababishi vya ugonjwa huu
👉 Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu
👉mawazo na huzuni kwa muda mrefu
👉kutokuwa na muda maalum wa kula
👉Utumiaji wa pombe uliopitiliza 
👉 Utumiaji wa madawa ya kulevya nk
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi ila sio wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo
👉maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (EPIGASTIC PAINS)
👉kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi Hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara
👉kutapika damu
👉mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula
👉mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa na akil hupata afueni
👉kupoteza hamu ya kula
👉kupata haja kubwa yenye raha ya damu Tena chenye harufu mbaya
👉kupungua uzito
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
~matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatzo ni tiba yenyew kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatzo mengine kutokana na matibabu yenyew kuhusisha mfumo wa dawa za kemikal ambazo Zina madhara kwa mhusika na pia Zina maudhi mengi hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa ziszo na kemikal pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti
MAMBO YA  KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
👉epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau nk
👉 epuka kutumia pombe
👉epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
👉kula Chakula kidogo kwa muda maalum
👉kula vyakula vyenye fiber yan vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga
👉tengeneneza juice juice ya kabichi na karoti ni tiba Tosha ya vidonda vya tumbo
👉epuka unywaji wa kahawa au kinywaj chochote chenye caffeine kiepuke
👉epuka vyakula vyenye ngano
HABARI NJEMA KWENU TUNATOA TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO
KAMA UNASUMBULIWA NA UGONJWA HUU 0757157702 WASILIANA NAMI UJIPATIE DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Health & Business Consultant Francis Kulwa has been added to your page

TOTAL PAGE VIEWERS

Live Traffic Feed

Health & Business Consultant Francis Kulwa

INSTAGRAM

Instagram
francis kulwa. Powered by Blogger.

Recent Posts

Unordered List

Theme Support